Matokeo darasa la saba 2016 haya hapa bonyeza hapo link BONYEZA HAPA KUYAPATA karibu saaana endelea kuwa nasi Whatsap :: 0758244348 YouTube :: kisleu fahari
Habaribado hujachelewa haya >>HAPA matokeo kidato cha NNE mwaka 2015/016 bila chenga karibu endelea kuwa nasiiiiiii kwa taarifa nyingine zaidi ..... bonyeza neno HAPA kuyafikia usisubiri wakuangalizie tupate kupia ...... whatsApp 0758244348 au Facebook //kisleu Eliya instagram @kisleufahari
***SIMULIZI YENYE MAZINGATIO*** ...Aboubakar ni mwajiriwa katika kampuni moja ya usambazaji wa nyama. Siku moja jioni baada ya kumaliza kazi zake za siku aliamua aingie katika chumba baridi cha kuhifadhia nyama kukagua kitu na kwa bahati mbaya mlango ukajifunga huku akiwa ndani. Alijaribu kugonga mlango na hata kupiga kelele za kuomba msaada kwa muda mrefu lakini jitihada zake hazikufanya lolote kwani kutokana na barafu zilizomo ndani na jinsi.........................ENDELEA MBELE kulivyozibwa kuzuia ubaridi kutotoka nje haikuwa rahisi kilio chake cha kuomba msaada kusikika. Haikuwa rahisi kusikika sauti yake kutoka katika chumba hicho na kila mfanyakazi alikuwa ameshaondoka. Masaa manne baadae Aboubakar alikuwa kama yuko katika bonde la umauti akisubiri kifo chake huku akimwomba Mungu wake kwa sala yenye unyenyekevu mkubwa. Akiwa katikati ya sala yake mara akashtushwa kuona mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na mlinzi wa kampuni hiyo akiingia na kumwokoa. Wakiwa katika chumba kingine huku Aboubakar akiwa kapewa msaada wa moto ili kuupasha mwili wake joto na kahawa ikiwa Mezani, Aboubakar akaamua amuulize yule mlinzi ni kitu gani kilimfanya akifungue chumba kile. Mlinzi akamjibu, " nimefanya kazi katika kampuni hii kwa miaka 21 na katika kipindi hiki mamia ya wafanyakazi wamekuwa wakiniona kama mtu nisiye na maana na ni wachache sana wanaonisalimia kwa kuniambia HABARI ZA ASUBUHI wakiwa wanaingia kazini na KAZI NJEMA wanapoondoka jioni kurudi makwao. Leo asuhuhi ulipoingia ulinisalimia kwa furaha kama kawaida yako na jioni wakati watu wanaondoka kurudi kwao nikaisubiri sauti yako kunifariji tena kwa kusema KAZI NJEMA kama siku nyingine lakini sikuisikia ndio nikaamua kuanza kupitia kila chumba kuona nini kimekupata na ndio nikakuona kwenye chumba kile ukiwa umefungiwa" Aboubakar kwa furaha yenye maumivu alibubujikwa na machozi katika macho yake. Funzo Mthamini aliyejuu na aliye chini yako, kwani yajayo huyajui, bali unayajua yalopita tuu. Tuishi maisha ya kupendana na kuwajali wale watuzungukao kwani huwezi jua ni namna gani kwa kufanya hivyo tunawapa furaha katika maisha yao na kuwafariji. UPENDO NI NGUZO MUHIMU KTK MAISHA By.. kisleu.com
KWA JINA NAITWA KISLEU FAHARI YA ELIYA NAPENDA KUKU KARIBISHA EWE MWANA BLOG NA MPENDA AMANI KATIKA BLOG HII ILI TUWEZE KUSHERE PAMOJA YALE TUNAYO YAPATA KARIBUNI
YATAKUWEPO MASIMULIZI MBALI MBALI KUTOKA KWA WATU WALIO PITIA MIKASA YA MAISHA BILA KUSAHAU NYIMBO NA MATUNZI MENGI KUTOKA WASANII WETU WAMTAANI